Luke 15

1Basi watoza ushuru wote na wengine wenye dhambi walikuja kwa Yesu na kumsikiliza. 2Mafarisayowaote na waandishi wakanung’unika wakisema, “Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi na hata hula nao.”

3Yesu akasema mfano huu kwao, akisema 4“Nani kwenu, kama ana kondoo mia moja na akipotelewa na mmoja wao, hatawaacha wale tisini na tisa nyikani, na aende akamtafute yule aliyepotea hadi amwone? 5Naye akisha kumpata humweka mabegani pake na kufurahia.

6Afikapo kwenye nyumba, huwaita rafiki zake na jirani zake akawaambia furahini pamoja nami, kwa kuwa nimempata kondoo wangu aliyepotea.’ 7nawaambia vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, zaidi ya wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu

8Au kuna mwanamke gani mwenye sarafu kumi za fedha, akipotewa na sarafua moja, hata washa taa na kufagia nyumba na kutafuta kwa bidii hadi atakapoipata? 9Na akiisha kuiona huwaita rafiki zake na jirani zake akawaambia furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena sarafu yangu niliyokua nimeipoteza. 10Hata hivyo nawaambia kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.”

11Na Yesu akasema, “Mtu mmoja alikua na wana wawili 12yule mdogo akamwambia babaye, Baba nipe sehemu ya mali inayonistali kuirithi. Hivyo akagawanya mali zake kati yao.

13Siku si nyingi yule mdogo akakusanya vyote anavyomiliki akaenda nchi ya mbali, na huko akatapanya hela zake, kwa kununua vitu asivyo vihitaji, na kutapanya fedha zake kwa anasa. 14Nae alipokua amekwisha tumia vyote njaa kuu iliingia nchi ile naye akaanza kuwa katika uhitaji.

15Akaenda na kujiajiri mwenyewe kwa mmoja wa raia wa nchi ile, naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe. 16Na akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe kwa sababu hakuna mtu aliempa kitu chochote apate kula.

17Ila yule mwana mdogo alipozingatia moyoni mwake, alisema ‘ni watumishi wangapi wa baba yangu wanachakula kingi cha kutosha na mimi niko hapa, ninakufa na njaa! 18Nitaondoka na kwenda kwa baba yangu, na kumwambia, “Baba nimekosa juu ya mbingu na mbele ya macho yako. 19Sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.”

20Ndipo akaondoka akaenda kwa baba yake. Alipokua angali mbali baba yake alimuona akamwonea huruma akaenda mbio na kumkumbatia na kumbusu. 21Yule mwana akamwambia, ‘baba nimekosa juu ya mbingu na mbele ya macho yako sistahili kuitwa mwana wako.’

22Yule baba aliwaambia watumishi wake, ‘lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike mtieni na pete kidoleni na viatu miguuni. 23Kisha mleteni ndama yule alienona mkamchinje tule na kufurai. 24Kwa kuwa mwanangu alikua amekufa naye yu hai. Alikua amepotea nae ameonekana wakaanza kushangilia.

25Basi yule mwanae mkubwa alikuwako shamba. Alipokuwa akija na kuikaribia nyumba alisikia sauti ya nyimbo na michezo. 26Akaita mtumishi mmoja akamuuliza mambo haya maana yake nini? 27Mtumishi akamwambia mdogo wako amekuja na baba yako amemchinjia ndama aliyenona kwa sababu amerudi salama.’

28Mwana mkubwa akakasirika akakataa kuingia ndani na babaye alitoka nje kumsihi. 29Ila akamjibu babayake akisema, ‘Tazama mimi nimekutumikia miaka mingi, wala sijakosa amri yako, lakini hujanipa mwana mbuzi, ili niweze kusherehekea na rafiki zangu. 30Lakini alipokuja huyu mwana wako aliyetapanya mali yako yote pamoja na makahaba umemchinjia ndama alienona.

31Baba akamwambia, ‘Mwanangu, wewe u pamoja nami siku zote na vyote nilivyo navyo ni vyako. Ila ilikua vyema kwetu kufanya sherehe na kufurahi, huyu ndugu yako alikua amekufa, na sasa yu hai; alikua amepotea naye ameonekana.”

32

Copyright information for SwaULB